• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM watoa wito wa kupambana na ubaguzi wa aina zote

    (GMT+08:00) 2020-07-21 09:04:32

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameitaka jamii ya kimataifa kuboresha haki na kupambana na aina zote za ubaguzi.

    Akizungumza jana katika Mkutano wa Baraza Kuu la Kumbukumbu ya Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela, Bw. Guterres amesema, kila siku, katika kazi za Umoja huo duniani, ni lazima wachukue nafasi yao katika kuhimiza haki, heshima na ushirikishi, na kupambana na ubaguzi wa aina zote.

    Amesema wakati dunia inapomkumbuka Mandela na mapambano yake ya muda mrefu kwa ajili ya haki na usawa, inapaswa kutambua kuwa bado dunia inakabiliwa na adha kubwa ya ubaguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako