• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya Deni la Kitaifa lilifika Sh6.6 trillion mwezi Mei

  (GMT+08:00) 2020-07-21 20:00:48

  Deni la Kitaifa la Kenya liliongezeka kwa Sh212.82 bilioni mwezi Mei kutoka mwezi uliopita, kutokana na madeni yaliokopwa serikalini na wakopeshaji wa kimataifa ili kutuliza hali mbaya ya kiuchumi kutokana na janga la Corona.

  Takwimu kutoka Benki Kuu ya Kenya, inaonyesha kwamba deni ya serikali ilisimamia Sh6.649 trilioni mwishoni mwa Mei, ambayo inajumuisha deni la nje la Sh3.496 trilioni na Sh3.153 trilioni katika kukopa ndani.

  Mnamo Aprili, deni hilo lilirekodiwa kuwa Sh6.436 trilioni, na kuongezeka Mei kwa kiasi kikubwa juu ya mikopo ya nje, ambapo kulikuwa na ongezeko la Sh179.1 bilioni.

  Deni la ndani wakati wa mwezi huo iliongezeka na Sh33.7 bilioni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako