• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya Kampuni ya China Stecol imepata mkataba wa Sh5.6 bilioni

    (GMT+08:00) 2020-07-21 20:01:07

    Kampuni ya China Stecol imepata mkataba ya Sh5.6 bilioni kuanza ujenzi wa barabara za kipekee kwa mabasi yenye uwezo mkubwa kupitia jijini Nairobi na barabara kuu ya Thika mwezi ujao.

    Mradi huu unatarajiwa kusaidia huduma za umma za jiji na kusaidia kupunguza msongamano wa trafiki

    Mradi huo utajumuisha mabasi zaidi ya 100 yatakayo fanya kazi kwenye barabara hizi za kipekee kwenye barabara kuu ya Thika kupitia jiji la Nairobi kuelekea eneo la Hospitali ya Kitaifa ya Kenya (KHN).

    Kila basi inatarajiwa kuwa na uwezo wa abiria wapatao 160 ambao watatumia kadi za elektroniki kwa malipo katika vituo vya basi.

    Benki ya Dunia inakadiria kuwa wakazi wa Nairobi kwa wastani hutumia saa moja kusafiri kwenda kazini na dakika nyingine 60 kurudi nyumbani kwa sababu ya msongamano wa magari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako