• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Klabu ya Fenerbahce yamkodolea macho Mbwana Samatta

    (GMT+08:00) 2020-07-22 17:26:26

    Kwa mujibu wa gazeti la habari za michezo la Nchini Uturuki la Takvim limeripoti kuwa klabu ya Fenerbahce ya Uturuki inavutiwa na mshambuliaji mpya wa Aston Villa ya England, Mbwana Samatta. Mshambuliaji huyo raia wa Tanzania alijiunga na Villa katika dirisha la usajili lililopita akiwa chaguo la kwanza ili kuziba pengo la Mbrazil, Wesley aliyekuwa akisumbuliwa na majeraha. Samatta ameshindwa kuleta mafanikio ndani ya Aston Villa katika michezo yake ya Premier League baada ya kufunga goli moja 1 pekee katika michezo 12 aliyocheza. Kwa mujibu wa Takvim, Fenerbahce inakaribia kumnasa Samatta kutokana na hali iliyopo kwa sasa ndani ya Aston Villa na itawakilisha ofa yake ya kumchukua kwa mkopo kutoka katika klabu hiyo ya Birmingham. Inadaiwa yapo makubaliano ya maneno baina ya Samatta na Villa kuwa Aston Villa itatakiwa kumruhusu kujiunga na klabu nyingine endapo timu hiyo haitafanikiwa kuwepo Premier League katika msimu ujao. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 pia amehusishwa na wapinzani wa Fenerbahce ambayo ni timu ya Galatasaray kutoka Uturuki ikihitaji huduma yake. Mkataba wa Samatta ndani ya Aston Villa utafikia tamati mwezi Juni mwaka 2024.

    Wakati huohuo Aston Villa imeanza kurejesha matumaini ya kubaki ndani ya Ligi hiyo baada ya usiku wa kuamkia leo kushinda bao 1-0 mbele ya Arsenal. Bao pekee la ushindi lilifungwa na Mahmoud Ahmed Hassan maarufu kama Trezeguet dakika ya 27 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huku mashabiki wa Arsenal wakimshushia lawama nyota wao Pierre Emerick Aubameyang kwa kushindwa kutimiza majukumu yake. Ushindi huo unaifanya Villa kufikisha pointi 34 ikiwa nafasi ya 17 huku vita vya kushuka ikiwa ni dhidi ya Watford na Bournemouth ambao wote wamecheza mechi 37 na pointi ni 34 hivyo ili kujihakikishia nafasi ya kubaki inatakiwa ishinde mchezo wa mwisho dhidi ya West Ham United utakaopigwa Julai 26.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako