• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Mauzo ya maua yaanza kurejea kawaida soko la Ulaya

    (GMT+08:00) 2020-07-22 17:56:16

    Mauzo ya maua ya Kenya yameendelea kuongezeka huku mahitaji katika soko la ulaya yakifikia asilimia 85 na kuongezea matumaini kuwa sekta hiyo inaweza kurejea hali ya kawaida mwaka ujao.

    Wakulima wa Kenya walilazimika kutupa maelfu ya tani za maua tangu Machi wakati Ulaya ilifunga shughuli za mikusanyiko kama vile harusi na mazishi.

    Lakini sasa mtendaji mkuu wa Baraza la Maua la Kenya Clement Tulezi amesema mahitaji yameanza kurejea yanarudi huku ufunguaji ukianza na vikwazo kupungua kwenye masoko muhimu.

    Ulaya hununua asilimia 70 ya maua ya Kenya lakini kutokana na janga la corona ilipunguza uagizaji kwa kwa nusu, na kutishia maelfu ya ajira.

    Maua ni mojawepo wa bidhaa zinazoletea Kenya mapato mengi ya kigeni na iliiletea nchi hiyo dola bilioni 1 mwaka 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako