• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Wakulima wa mboga Arusha kunufaika na mkataba mpya

  (GMT+08:00) 2020-07-22 17:56:46

  Wizara ya Kilimo ya Tanzania imeingia mkataba wa miaka 10 na Kampuni ya AVRDC The World Vegetable Center ya Tengeru mkoani Arusha, ili kufanya utafiti wa mbegu bora za kilimo cha mbogamboga na kuinua sekta hiyo.

  Imesema lengo la kufanya hivyo ni kutaka sekta hiyo ichangie pato la taifa kwa kiwango kikubwa kama zilivyo sekta nyingine.

  Katika hafla ya utiaji saini mkataba huo, Katibu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya, alisema ameagiza ziundwe kamati ndogo kwa ajili kusimamia mpango huo.

  Alisema kutokana na hatua hiyo, serikali itakwenda kusimamia utafiti huo ili kuimarisha mpango huo ambao una malengo mazuri.

  Alisema pia wanakwenda kuimarisha vyuo vya kilimo pamoja na taasisi nyingine zilizochini ya TARI, ili kusaidia kukuza mpango huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako