• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan, Ethiopia na Misri zakubaliana kuendelea na mazungumzo kuhusu kujaza maji kwenye bwana kubwa la Ethiopia

    (GMT+08:00) 2020-07-22 17:57:10

    Waziri Mkuu wa Sudani Abdalla Hamdok alitangaza kwamba nchi yake, Ethiopia na Misri zimefikia makubaliano ya kuendelea na mazungumzo kuhusu kujaza maji kwenye bwana kubwa la Ethiopia (GERD).

    Makubaliano hayo yamefikia baada ya mkutano ulioitishwa na Umoja wa Afrika ambao ulihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, mwenyekiti wa Tume ya AU Moussa Faki Mahamat na mwenyekiti AU, Cyril Ramaphosa.

    Waziri mkuu wa Ethipoa Abiy Ahmed kwa upande wake aliezea kuridhishwa kwake na makubaliano hayo ya kuendelea na majadiliano ya kiufundi kuhusu kujaza maji bwawa hilo.

    Ethiopia ilianza kujenga bwawa lake hilo kubwa mwaka 2011, lakini Misiri na Sudan zimekuwa zikilalama kuwa litaathiri kiwango cha maji kwenye mto Nile ambao ndio tegemeo lao la kilimo.

    Ethiopia inasema bwawa hilo linatoa fursa muhimu ya kuondoa zaidi ya watu 110 kutoka kwa umaskini na pia kuwa muuzaji mkubwa wa umeme.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako