• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: TPSF yawahahakishia wanachama itaendelea kushirikiana na serikali

    (GMT+08:00) 2020-07-22 17:58:18

    Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), imewahakikishia wanachama wake wote kuwa itaendelea kuwa kiungo muhimu kwa wadau wote ikiwemo sekta ya umma sambamba na kufanikisha mageuzi ya kiuchumi na kijamii yanayoendelea nchini.

    Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Angelina Ngalula na kwamba TPSF ipo imara na itaendelea kushirikiana na serikali katika kuwaletea Watanzania maendeleo ya kiuchumi.

    Ngalula alisema taasisi hiyo itaendelea kutumia fursa zote ambazo zinapatikana ndani na nje ya nchi na kuwafanya wadau wake wazidi kunufaika kwa kutanua masoko la bidhaa zinazozalishwa na wadau wake, kuhamasisha na kukuza uwekezaji hapa nchini.

    Aidha, aliwasihi wadau wa TPSF kuzidi kuungana hasa katika kipindi hiki ambacho taasisi hiyo imefanya mabadiliko ya kiuongozi baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Godfrey Simbeye kumaliza muda wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako