• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • COVID-19 yasababisha hasara ya biashara ya kikanda kwa asilimia 40 EAC.

  (GMT+08:00) 2020-07-23 19:06:10

  Mlipuko wa janga la Corona unaendelea kuhatarisha biashara ya kikanda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki,na kuirejesha nyuma kwa asilimia 40.

  Haya ni kwa mujibu wa Shirika la TradeMark East Africa,TMEA.

  Baada ya mlipuko ,serikali za kanda zilianzisha kanuni za kudhibiti utembeaji wa watu mipakani ,na kuruhusu tu usafrishaji wa bidhaa na mizigo.

  Katika utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na TMEA,vikwzo vya kuzuia watu kutembea pia vilipunguza shughuli za wafanyabishara wasio rasmi mipakani ambao kwa kiwango kikubwa wanachangia katika biashara ya kikanda.

  Wafanyabiashara wa mipakani ,ambao kwa kawaida wengi wao huwa ni wanawake,wanachangia takriban asilimia 60 kwa biashara katika mipaka ya JUmiya ya Afrika Mashariki.

  TMEA imesema kuwa tangu mlipuko wa janga la Corona,wenye viwanda katika kanda pia wameamua kushughulika na masoko ya ndani na kuacha tu bidhaa za kilimo kuvuka mipaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako