• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hakuna uhaba wa mafuta Tanzania,wala hayataadimika,yasema PBPA

    (GMT+08:00) 2020-07-23 19:06:33

    Wakala wa Uagizaji Mafuta Pamoja Tanzania (PBPA), umesema kuna akiba ya kutosha ya mafuta nchini humo na kuwataka Watanzania wasitarajie kuona upungufu kutokana na mifumo thabiti waliyoweka.

    Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PBPA, Erasto Mulokozi, alisema hayo jana alipokuwa akizungumzia mafanikio na changamoto tangu kuanzishwa kwa mfumo huo mpya wa kuagiza mafuta mwaka 2015.

    Alisema wamekuwa wakifuatilia kwa karibu matumizi ya mafuta kila siku na akiba iliyopo, hivyo suala la uhaba wa nishati hiyo haliwezi kutokea kwa mfumo waliojiwekea wa ufuatiliaji.

    Mulokozi alisema hata maneno yaliyotokea hivi karibuni kwamba baadhi ya mikoa ilikuwa na upungufu wa mafuta, ulikuwa uzushi na hila za baadhi ya waagizaji na ndiyo sababu Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) iliingilia kati na kulimaliza.

    Alisema kanuni inataka kila kampuni ya mafuta iwe na akiba ya kujiendesha kwa siku 15 mbele lakini PBPA imekwenda mbali zaidi kwa kuweka hadi siku 40 ili kuhakikisha mafuta ya akiba yanakuwapo hata meli yenye shehene mpya ikichelewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako