• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hitaji kubwa la U$ lafanya shilingi ya Kenya kushuka na kubadilishwa kwa Ksh.108

  (GMT+08:00) 2020-07-23 19:08:15

  Sarafu ya Kenya imeendelea kuwa na utendaji mbaya baada ya kubadilishwa kwa Silingi 108 dhidi ya dola 1 ya Marekani jana.

  Benki Kuu ya Kenya ilitangaza kiwango cha ubadilishanaji cha Ksh.108.12 dhidi ya dola ya Marekani jumatano,huku shilingi ya Kenya ikionekana kuchukua mwenendo wa kushuka thamani kutoka ubadilishanaji wa Ksh 100.21 mwanzoni mwa mwezi Februari.

  Katika tangazo lake la kila wiki,Benki Kuu ya Kenya ilisema kushuka huko kwa thamani kumetokana na hitaji kubwa la dola za Marekani katika soko la baina ya benki na benki.

  Wachambuzi wa masuala ya fedha hata hivyo wana maoni mseto kuhusu kushuka thamani kwa sarafu ya Kenya ,jambo lililozua wasiwasi katika soko la ubadilishanaji wa fedha za kigeni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako