• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wafanya biashara wa samaki aina ya dagaa waomba msaada

  (GMT+08:00) 2020-07-24 18:14:23

  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanya biashara wa Dagaa wa eneo la Mangapwani, Tanzania Bw Mohammed Omar Makame ameiomba serikali kuwasaidia kukabiliana na changamoto zinazowakabili ikiwemo ya kuwajengea sehemu ya kuhifadhia bidhaa zao.

  Omar amesema kutatuliwa kwa changamoto hizo kutawasaidia kupata sehemu ya kuanika dagaa zao pamoja na kupata sehemu ya uhakika ya kuhifadhi mizigo yao.

  Pia ameongeza kuwa hivi sasa wanakabiliwa na tatizo la majisafi na salama na uchache wa vyoo vya kudumu, jambo ambalo linahatarisha usalama wa afya zao.

  Mwenyekiti huyo aliomba serikali kuangaliwa upya bei elekezi ya dagaa kama iliyowekewa katika zao la mwani na kuwashauri wapishi wa dagaa kuweka mfumo wa kutumia majiko ya gesi ili kuhifadhi mazingira.

  Pamoja na hayo, aliomba serikali kuwapatia mikopo isiyo na riba ili kuwasaidia kujinyanyua zaidi kimaisha kwa kufanya biashara itayoweza kuwanyanyua zaidi na kujiendeleza kimaisha bila ya kuhitaji msaada.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako