• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Barakoa na sanitaiza feki zafurika sokoni

  (GMT+08:00) 2020-07-24 18:14:51

  Huku idadi ya wahudumu wa afya wanaoambukizwa virusi vya corona nchini Kenya ikiongezeka, imebainika kuwa serikali imekuwa ikiuziwa vifaa feki vya kujikinga (PPEs).

  Shirika la serikali la kupambana na bidhaa feki (ACA) limesema limeanza oparesheni ya kuwasaka wafanyabiashara wanaoagiza, kutengeneza na kuuza vifaa hivyo feki.

  ACA ilisema hayo wakati Wizara ya Afya ikitangaza visa vipya 796 vya maambukizi ikiwa idadi kubwa zaidi kuripotiwa kwa siku moja nchini.

  Wizara ya Afya ilisema kuna jumula ya visa 15,601 nchini vya maambukizi ya corona.Kulingana na shirika la ACA, baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiuza sanitaiza na barakoa ambazo ni za ubora wa chini.

  Hali hii imetajwa kama mojawapo za sababu zinazolemaza vita dhidi ya virusi vya corona kote nchini huku idadi ya maambukizi ikizidi kupanda.A

  fisa Mkuu Mtendaji wa ACA, Elema Halake, jana alisema kikosi cha kupambana na wafanyabiashara wakora kinaendelea kuzunguka kote nchini na kitashirikiana na serikali za kaunti kuwanasa wenye kampuni zinazotengeneza sanitaiza na barakoa feki. Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, amekuwa akisema serikali ina uwezo wa kutengeneza vifaa vya kujikinga na virusi vya corona vya ubora wa juu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako