• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wafanyabiashara wadogo wadogo Tanzania walalamikia kodi

  (GMT+08:00) 2020-07-24 18:15:12

  Wafanyabiashara wadogo wadogo wa mboga na matunda katika soko la Lembuka, mkoani Mbeya nchini Tanzania wamelalamika kuwa licha ya kununua vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na Rais Dk. John Magufuli, bado wilaya hiyo, inaendelea kuwatoza kodi.

  Wanasema licha ya kuwa na vitambulisho kama agizo la Rais bado wanaendelea kutozwa ushuru wa mazao usiozidi tani moja.

  Wameongeza kuwa kutokana na hali hiyo hawaoni umuhimu wa vitambulisho hivyo kwa vile Halmashauri yao inaendelea kuwatoza ushuru kinyume na maelekezo waliyopewa kabla ya kununua vitambulisho hivyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako