• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka ya kodi Kenya yapaya hasara ya bilioni 1 kila mwezi kutokana na Covid 19

    (GMT+08:00) 2020-07-24 18:15:38

    Mamlaka ya kodi ya Kenya KRA inadaiwa kupata hasara ya karibu shilingi bilioni 1 kila siku kutokana na janga la corona. Mamlaka hiyo imesema hasara hiyo ambayo imedumu miezi mitatu hivi sasa inatokana na kupunguzwa kwa kodi ikiwa ni hatua ya serikali ya kuwapunguzia mzigo wakenya wakati huu wa janga la corona. Kuanzia mwezi wa tatu mwaka huu hadi mwezi wa juni KRA imekusanya jumla ya bilioni 333.46 ikiwa ni chini ikilinganishwa na bilioni 419.90 zilizokusanywa kipindi kama hicho mwaka jana. Sababu zingine ambazo zimechangia kupungua kwa makusanyo ya kodi ni kufungwa kwa biashara nyingi kutokana na kukosekana kwa wateja, watu wengi kuachishwa kazi na wengine kupunguziwa mishahara. Aprili mwaka huu serikali ya Kenya ilipunguza kodi kutoka asilimia 30 hadi 25 kama juhudi za kuwapunguzia mzigo wakenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako