• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AFRIKA: FACEBOOK KUINUA UCHUMI WA AFRIKA KWA KUWEKEZA DOLA BILIONI 57 KWA MIAKA MITANO IJAYO

  (GMT+08:00) 2020-07-27 15:35:39

  Habari njema kwa bara la Afrika ni kwamba mtandao wa Facebook unapania kuwekeza dola bilioni 57 katika miundo msingi na uunganishaji wa mtandao kwa miaka mitano ijayo. Utafiti huu mpya unaonyesha kwamba hatua hii itainua uchumi wa bara la Afrika kwa kiasi fulani.

  Hii si mara ya kwanza kwa Faceook kuwekeza barani Afrika. Kwa miaka mingi, mtandao huu umekuwa ukiwekeza kwenye miundo msingi na kushirikiana na mashirika mbali mbali ili kurahisisha upatikanaji wa mtandao kwa mataifa ya ASfrika.

  Utafiti unaonyesha kuwa takriban watu milioni 800 barani Afrika hawana uwezo wa kutumia mtandao. Vile vile, Facebook itashirikiana na kampuni za simu za mkononi na zile za mawasiliano kufikia malengo yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako