• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • DUNIANI: Maskini walipwe kipato cha msingi kila mwezi kuepusha COVID-19- UNDP

  (GMT+08:00) 2020-07-27 15:36:11

  Umoja wa Mataifa umesema kuwa kuwapatia watu maskini zaidi duniani kipato cha kujikimu, TBI, kunaweza kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona.

  Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP katika ripoti yake iliyochapishwa mwishoni mwa wiki jana, limesema kuwa kipato hicho kitawezesha watu takribani bilioni 3 kusalia nyumbani badala ya kutoka kwenda kusaka ajira ili kukimu familia.

  Ikipatiwa jina Kipato cha msingi cha muda, kulinda watu walio hatarini zaidi katika nchi maskini, ripoti hiyo inakadiria kuwa mpango huo utagharimu dola bilioni 199 kwa mwezi na utalinda watu bilioni 2.7 kote duniani kwenye mataifa 132 yanayoendelea.

  Ripoti inaeleza kuwa mpango huo unawezekana na unatakiwa haraka wakati huu ambapo janga la Corona linasambaa kwa kasi.

  Inachambua takwimu hizo ikisema kuwa katika watu hao, 7 kati ya 10 ni wafanyakazi katika sekta isiyo rasmi ambao hawawezi kupata kipato iwapo watasalia nyumbani wakijikinga dhidi ya Corona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako