• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapenzi wa soka Tanzania kuendelea kumfuatilia Samatta lihi kuu ya Uingereza

    (GMT+08:00) 2020-07-27 17:27:19

    Wapenzi wa soka nchini Tanzania wataendelea kumwona kijana mtanzania Mbwana Ally Samatta akiwa na kikosi cha Aston Villa kilichoinusuru timu hiyo kushuka daraja, baada ya sare ya 1-1 na wenyeji West Ham United Uwanja wa London. Katika mchezo huo uliochezwa jana Samatta alicheza kwa dakika 68 mchezo huo wa Ligi Kuu ya England kabla ya kumpisha chipukizi wa England, Keinan Davis wakati huo timu hizo hazijafungana. Nyota wa England, Jack Grealish alianza kuifungia Aston Villa dakika ya 84 akimalizia pasi ya kiungo mwenzake, Mscotland John McGinn bao lililodhaniwa litakuwa la ushindi. Lakini mshambuliaji wa kutoka Ukraine Andriy Yarmolenko aliisawazishia goli West Ham United katika dakika ya 85 akimalizia pasi ya kiungo wa England, Declan Rice. Kwa matokeo hayo, Aston Villa imekamilisha msimu wa Ligi Kuu ya England na pointi 35, ikizizidi pointi moja moja AFC Bournemouth na Watford zilizoungana na Norwich City kushuka daraja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako