• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafunga ubalozi mdogo wa Marekani mjini Chengdu kwa haki

    (GMT+08:00) 2020-07-27 19:50:39

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, China kutaka Marekani ifunge ubalozi mdogo wake mjini Chengdu na kuukabidhi kwa China ni jibu la haki na lazima kwa hatua ya Marekani ya kufunga ubalozi mdogo wa China mjini Houston na kuingia kwenye ubalozi huo kwa nguvu.

    Bw. Wang amesema hatua hiyo ya China inafuata sheria za kimataifa, kanuni ya kimsingi ya uhusiano wa kimataifa, na utaratibu wa kidiplomasia. Amesisitiza kuwa China haipendi kuona hali hiyo iliyosababishwa na Marekani na kuitaka Marekani kusahihisha makosa yake, ili kuanzisha mazingira ya lazima kwa ajili ya kurejea kwa uhusiano wa kawaida kati ya nchi hizo mbili.

    Alipotaja kauli ya Marekani inayodai kuwa ubalozi mdogo wa China mjini Houston ulifanya uhalifu wa kuiba siri za kibiashara na vitendo vya ujasusi, Bw. Wang amesema kauli hiyo haina msingi wowote, ni wongo na kuipaka matope China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako