• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eymael aeleza sababu za kukasirika na kutoa lugha chafu dhidi ya Yanga na mashabiki wake

    (GMT+08:00) 2020-07-28 17:48:07

    Kocha mbelgiji ambaye jana alitimuliwa na Yanga kutokana na matumizi ya lugha chafu na lugha ya kibaguzi, amesema alifanya hivyo kutokana na hasira, hasa baada ya kuona kuwa timu yake imeshindwa kupata ushindi dhidi ya timu ya Mtibwa sugar, na kulazimishwa sare ya goli moja kwa moja. Malalamiko yake ni kuwa alikuwa akirushiwa lugha ya matusi na mashabiki kutokana na kutoleta matokeo mazuri kwenye timu hiyo, na kuona kuwa marefa hawajui kuchezesha mechi. Hata hivyo Mwinyi Zahera aliyewahi kuwa kocha wa Yanga amemlaani sana kocha huyo kwa lugha yake ya kibaguzi, na kusema ana bahati sana kupata mshahara wa dola elfu 6 nchini Tanzania, kwani barani Ulaya hawezi hata kupata mshahara wa dola elfu mbili. Amesema amesikitishwa sana na kitendo chake kwa kuwa kutokana na mshahara mkubwa anaolipwa, alitakiwa kuwa na adabu na hakutakiwa kuwa na lugha chafu kama hiyo.

    Habari nyingine zinasema kocha mkuu wa timu ya Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema hayuko tayari kujiunga na Yanga ambayo imesema iko tayari kumpa mshahara wa Shilingi Milioni 8 na marupurupu mengine ili ajiunge na timu hiyo. Maxime ameishukuru Yanga kwa kuwaambia 'asante' na kwamba atabakia Kagera Sugar kwani anaridhika na maisha ya kuifundisha timu hiyo ya Bukoba Mjini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako