• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Simba yaanza kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao

    (GMT+08:00) 2020-07-28 17:48:32

    Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Rayon Sports ya Rwanda, Michael Sarpong, amesema anasubiria viongozi wa Simba wamtumie tiketi ili aweze kuja Tanzania na kusaini mkataba ili aweze kunichezea timu hiyo.

    Sarpong, raia wa Ghana, inaelezwa amemalizana na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Rayon Sports ambayo iliamua kumtema kutokana na matatizo ya utovu wa nidhamu. Lakini habari zinasema kwa sasa kila kitu kiko sawa na anasubiria simu kutoka kwa viongozi wa Simba ili aje kukamilisha usajili na timu. Amesema kwa sasa ni klabu ya Simba ndiyo wanajua lini anaweza kwenda Tanzania pamoja na maneja wake kwa ajili ya taratibu nyingine… Wakati Simba ikitaka kumsajili Michael Sarpong imeelezwa kuwa nyota saba ndani ya Simba safari yao itakuwa imefika tamati kikosini hapo kutokana na sababu mbalimbali Wachezaji wanaotajwa kuondoka msimu ujao ni pamoja na Marcel Kaheza anayemchezea Polisi Tanzania, Mohamed Rashid anayechezea JKT kwa mkopo,Shiza Kichuya ambaye hajawa na nafasi kikosi cha kwanza tangu aliporejea akitokea nchini Misri, Tairone Santos raia wa Brazili hajawa chaguo la kwanza mbele ya Sven Vandenbroeck, Sharaf Shiboub kiungo huyu raia wa Sudan ambaye baada ya kurejea kutoka nchini kwao ambako alikwama kutokana na janga la Corona amekuwa adimu kuonekana kikosi cha kwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako