• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mgogoro wa Soka wanukia Kenya, baada ya FKF kuwakataa Mombasa

    (GMT+08:00) 2020-07-28 17:48:54

    Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) Nick Mwendwa amesema Chama cha Soka cha Kaunti ya Mombasa (MCFA), licha ya kupewa kibali cha kufanya shughuli za michezo na serikali ya Kenya, hakitambuliwi na wala sio sehemu ya FKF. MCFA imepewa leseni ya muda na Msajili wa Michezo na imetangaza nia yake ya kufanya uchaguzi ndani ya miezi mitatu kabla ya kujihusisha na FKF. Bw. Nick amesema hana tatizo kama MCFA inaendesha shughuli zao kwa njia yoyote ile, lakini ni wazi kuwa wao si sehemu ya FKF na FIFA. Amesema tayari wametoa taarifa kwa FIFA ambao ndio wakuu wa mambo ya soka. Mwendwa na FKF wamekuwa matatani kutokana na kuahirisha mara kwa mara uchaguzi wa FKF kwa sababu mbalimbali, hali inayofanya baadhi ya watu kulalamikia uendeshaji wa FKF uliokwambisha chaguzi za ngazi ya kaunti na taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako