• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchumi wa Afrika Kusini kupungua kwa asilimia 7.2% mwaka huu

  (GMT+08:00) 2020-07-29 19:22:39

  Shirika la Fedha la Kimataifa IMF linasema kuwa kuwa uwezekano mkubwa kwamba uchumi wa Afrika Kusini utapungua kwa asilimia 7.2% mwaka huu kwa sababu ya athari ya virusi vya corona.

  Aidha IMF imesema kuongezeka kwa ulipaji wa madeni kutaathiri ukuaji.

  Mapema wiki hii IMF iliidhinisha mkopo wa dola bilioni 4.3 za dharura kwa Afrika Kusini

  Mkopo huo wa IMF ni sehemu ya dola bilioni 7 ambazo Afrika Kusini inapanga kukopa kutoka kwa taasisi za fedha za kimataifa.

  Benki ya BRICS pia imepitisha mkopo wa dola bilioni 1, nayo Benki ya Maendeleo ya Afrika inasema itaikopesha serikali dola milioni 304, huku mMazungumzo na Benki ya Dunia yakiendelea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako