• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia: AfDB yaidhinisha dola milioni 25 kwa somalia

    (GMT+08:00) 2020-07-29 19:23:05

    Benki ya Maendeleo ya Afrika imesema imeidhinisha ruzuku ya karibu dola milioni 25.1 kwa Somalia ili kuongeza juhudi za serikali kupunguza athari za janga la COVID-19.

    AfDB imesema serikali itatumia fedha hizo kutekeleza majukumu matatu yaliyoingiliana na janga hilo na ambayo yataboresha mfumo wa afya, lishe bora na kinga ya kijamii.

    Somalia hadi sasa imethibitisha watu 3,178 kuambukizwa na COVID-19, waliofariki wakiwa ni 93.

    Mashirka ya Umoja wa Mataifa na washirika wake UN wamesema wameongeza fedha za kukabili janga hilo licha ya changamoto za kiutendaji kama vile wafanyikazi wengi wanaofanya kazi wakiwa mbali au katika mazingira yenye vikwazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako