• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Kampuni ya kilombero kuzalisha tani 27,000 za sukari

    (GMT+08:00) 2020-07-29 19:24:52

    Kampuni ya Sukari ya Kilombero nchini Tanzania imesema imejipanga kuzalisha tani 127,000 za sukari kwa msimu wa mwaka 2020/21, ili kuondoa uhaba wa sukari nchini.

    Meneja Biashara na Masoko wa kampuni hiyo, Warda Kimaro, alisema hayo alipokuwa akizindua pakiti mpya za sukari zenye ujazo wa kilo tano.

    Alisema mbali na uzalishaji huo, pia kwa kipindi hicho wamejiwekea lengo la kusaga miwa tani 1,328,445.

    Aidha, alisema kampuni inafanya jitihada kuhakikisha inazalisha sukari nyingi ili kuendana na mahitaji ya wateja kwenye soko.

    Alisema kampuni ina mpango kuhakikisha pakiti hiyo inapatikana maeneo yote nchini sambamba na pakiti za ujazo mwingine zilizoko kwenye soko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako