Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, kauli za baadhi ya wanasiasa wa Marekani haswa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Mike Pompeo zinazosema kwamba mawasiliano kati ya Marekani na China yameshindwa, haiheshimu historia na wala hailingani na ukweli.
Bw. Wang amesema China inawataka wanasiasa hao wa Marekani waache mawazo ya vita baridi, kuutazama uhusiano kati ya China na Marekani kwa usahihi, na kuacha mara moja kauli na vitendo vinavyoharibu uhusiano huo, ili kuanzisha mazingira ya lazima kwa ajili ya kurejea kwa uhusiano wa kawaida kati ya nchi hizo mbili.
Bw. Wang amesema uhusiano kati ya China na Marekani unahusisha neema, amani na utulivu duniani, na katika karibu miaka 50 iliyopita tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, mawasiliano na ushirikiano kati yao vimeendelea kukua na kupanuka, na kuwanufaisha sana wananchi wao.
Bw. Wang amesisitiza kuwa dunia ina rangi tofauti, ingawa China na Marekani zina mifumo tofauti ya kijamii, lakini zinaweza kuishi pamoja kwa amani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |