• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zawapima watu zaidi ya milioni 8.3 kufuatia kusambaa kwa kasi kwa janga la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-07-30 09:13:12

    Kituo cha Kuzia na Kukinga magonjwa cha Afrika, Africa CDC, kimetoa taarifa kikisema bara la Afrika hadi sasa limewapima watu zaidi ya milioni 8.3 kufuatia kusambaa kwa kasi kwa janga la COVID-19 katika nchi hizo.

    Taarifa hiyo imetolewa Jumatano na Mkurugenzi wa CDC John Nkengasong kwa njia video ambayo ilikuwa ikiangalia mikakati ya kiuchumi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wenye COVID-19 katika baadhi ya nchi za Afrika. Ameonya juu ya ongezeko hilo la idadi ya watu wenye virusi vya Corona, ambalo hadi sasa lipo kwenye asilimia 10.5 ikilinganishwa na idadi ya watu waliofanyiwa vipimo.

    Mwezi Juni Africa CDC ilieleza mpango wake wa kuwapimia COVID-19 watu zaidi ya milioni 10 katika miezi michache ijayo ikiwa ni sehemu ya Ushirikiano wa Bara wa kuharakisha Upimaji wa COVID-19, unaoongozwa na nguzo tatu ambazo ni upimaji, ufuatiliaji na matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako