• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Covid-19- Global Peace Foundation yaandaa Mkutano wa kujadili suluhu za kufufua uchumi

  (GMT+08:00) 2020-07-30 19:01:50

  Mamia ya washiriki kutoka sehemu mbalimbali za ukanda wa Afrika wamefanya mkutano kupitia mtandao wa intaneti ulioandaliwa na Wakfu wa Amani Duniani (Global Peace Foundation) ambao ulijadili suluhu za kufufuka kiuchumi kutoka kwenye janga la Covid-19.

  Mkutano huo wa siku mbili ulianza jana na kukamilika leo.

  Mkutano huo wa Global Peace Foundation uliwaleta pamoja washiriki zaidi ya 1,000 kutoka mashirika yasiyokuwa ya srikali,serikali,mashirika ya kijamii pamoja na vyombo vya habari kutoka Kenya,Tanzania,Nigeria,Marekani na Uingereza.

  Lengo lilikuwa ni kubadilishana uzoefu,huku msisitizo ukiwa kwa vijana kutoa fursa za kujiajiri ili kwenda sawa na mgogoro wa kiuchumi ulioletwa na janga la Corona.

  Baadhi ya waliozungumza katika mkutano ni pamoja na mfanyabiashara maarufu Dkt Manu Chandaria,Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa jijini Nairobi,Siddharth Chatterjee,Waziri wa Teknolojia na Mawasiliano Joseph Mucheru na Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la Habari la Standard Orlando Lyomu.

  Dkt Manu Chandaria alisema hali itakuwa tofauti sana baada ya janga la Corona.Alisema itawalazimu upunguza mahitaji na kutakuwa na watu wengi watakaopoteza ajira na hivyo itabidi watu wajitegemee wenyewe.

  Alisema mkutano huo umetoa nafasi ya kukaa chini kuzungumza,na kila mmoja kumuelewa mwenzake na kubadilishana uzoefu na majirani kama vile Tanzania,Rwanda,na Uganda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako