• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Gharama za sensa ya Kilimo Tanzania kupungua kwa asilimia 40 kutokana na matumizi ya teknolojia

  (GMT+08:00) 2020-07-30 19:02:15

  Gharama za sensa ya kilimo,mifugo na uvuvi nchini Tanzania, zinatarajiwa kupungua kwa asilimia 40 kutokana na matumizi ya teknolojia ya kisasa katika ukusanyaji na uchakataji wa takwimu.

  Sensa hiyo inatarajiwa kufanyika nchini humo kwa miezi miwili kuanzia Agosti 3 ,mwaka huu ,na matokeo yake yatatolewa ndani ya muda mfupi kutokana na matumizi hayo ya teknolojia.

  Mtakwimu Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Takwimu,NBS,Tanzania,Festo Mwemtsi,alisema hayo jana wakati wa ufunguz wa mafunzo ya wadadisi wa sensa ya kilimo,mifugo na uvuvi ya mwaka wa kilimo 2019/2020.

  Alisema matumizi ya teknolojia hiyo amabayo itahusisha vishikwambi (tablets) badala ya makaratasi ,itasaidia kupunguza gharama za uendeshaji kutoka Sh.bilioni 10 hadi Sh.bilioni 6.

  Aidha aliwataka wananchi kushirikiana na wadadisi kwa kutoa taarifa sahihi ambazo zitaiwezesha serikali kupanga mipango ya maendeleo endelevu katika sekta za kilimo , mifugo , na uvuvi .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako