• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Ulaya kujenga eneo salama la kufanya biashara katika mpaka wa Kenya na Uganda wa Busia

  (GMT+08:00) 2020-07-30 19:02:33

  Wanawake wanaofanya biashara za mipakani katika mpaka wa kenya na Uganda wa Busia huenda wakarejelea shughuli zao kufuatia tangazo la Umoja wa Ulaya kwamba umetoa €100,000 ili kuanzisha eneo salama la kufanyia baishara kwa ajili yao.

  Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Kenya ,Simon Mordue, alitoa tamko hilo baada ya kuzuru kituo cha mpakani cha Busia jana.

  Umoja wa Ulaya kwa ushirikiano na Shirika la TradeMark East Africa,walitoa nguo za kujikinga dhidi ya Corona kwa mamlaka za Uganda na Kenya mpakani hapo.

  Takriban asilimia 80 ya biashara zisizo rasmi za mpakani hufanywa na wanawake ambao wanazitegemea kama chanzo pekee cha kujiingia kipato.

  Mordue alisema japokuwa watu wantegemea biashara,zinafaa kufanywa katika mazingira salama,haswa katika kipindi hiki cha janga la Corona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako