• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya CRDB Tanzania yazindua mfumo mpya wa kidigitali wa kupokea maoni

    (GMT+08:00) 2020-07-30 19:03:28

    Benki ya CRDB nchini Tanzania imezindua mfumo mpya wa kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wateja wake kwa kidigitali ujulikanao kama QR Code ambao unawawezesha wateja kutoa maoni na ushauri kwa kutumia simu janja badala y kujaza kwenye makaratasi.

    Mfumo huo uliziduliwa hivi karibuni unaelezwa kuwa na ufanisi zaidi kuliko ule uliokuwa ukitumika awali.

    Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo ,Mkurugenzi wa CRDB,Kata ya Mbeya,Denis Moleka ,alisema mfumo huo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo kuboresha mifumo yake ya utoaji huduma kwa wateja.

    Moleka alisema kutokana na kukua kwa teknolojia ,mahitaji ya wateja yamekuwa yakiongezeka kila uchao,ndiposa benki hiyo ikatilia mkazo matumizi ya njia za kidigitali kwenye mpango mkakati wa biashara wa miaka mitano kuanzia 2018-2022.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako