• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutoa ruzuku ya maisha kwa watu wengi zaidi kutokana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-07-30 19:41:53

    Wizara ya Mambo ya kiraia na Wizara ya Fedha ya China zimetoa taarifa ya pamoja ikisema kwa kushikilia vigezo vilivyopo na kuhakikisha mfumo wa ruzuku kwa watu wenye kipato cha chini zaidi unaendelea kwa utulivu na uendelevu, China itaongeza watu wanaoweza kupata ruzuku hiyo.

    Naibu mkurugenzi wa idara ya misaada ya kijamii ya Wizara ya Mambo ya kiraia ya China Bw. Jiang Wei, amesema watu wenye ulemavu au magonjwa makubwa wa familia zenye kipato cha chini wanaweza kuomba ruzuku ya maisha ya kimsingi, na katika sehemu zilizoathiriwa zaidi na janga la COVID-19, vigezo vya kipato cha chini vinaweza kurekebishwa kwa kiasi kinachofaa.

    Aidha kutokana na taarifa hiyo vigezo vya umri wa watu waishio katika umaskini uliokithiri pia vimerekebishwa kutoka miaka 16 kuwa 18.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako