• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhusiano kati ya China na Marekani haupaswi kuwa nyenzo ya mtu binafsi ya kujitafutia maslahi

    (GMT+08:00) 2020-07-30 19:42:10

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin, amesema uhusiano kati ya China na Marekani unahusiana na neema ya watu wa nchi hizo mbili na amani na utulivu duniani, na haupaswi kuwa nyenzo ya mtu fulani au kundi fulani la kisiasa ya kujitafutia maslahi.

    Mwanadiplomasia mwandamizi wa zamani wa Marekani Bw. Charles Freeman, hivi karibuni amesema hotuba iliyotolewa hivi karibuni na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo inapotosha historia na ukweli, na kwa jumla sera ya Marekani ya kuwasiliana na China imepata mafanikio makubwa na kudumisha amani.

    Bw. Wang amesema hivi karibuni hotuba hiyo ya Bw. Pompeo imekosolewa na maofisa waandamizi wa amani, wataalam na vyombo vya habari, na hali hii inaonesha kuwa jaribio la kutotambua maendeleo yaliyopatikana katika uhusiano kati ya China na Marekani, na kuchochea mgogoro wa kiitikadi hakukubaliki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako