• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mfumo wa saitelaiti wa kuongoza mawasiliano duniani wa Beidou No.3 wa China wazinduliwa rasmi

  (GMT+08:00) 2020-07-31 17:43:25

  Sherehe ya uzinduzi wa mfumo wa saitelaiti wa kuongoza mawasiliano duniani wa Beidou No. 3 wa China imefanyika leo hapa Beijing.

  Rais Xi Jinping wa China amehudhuria sherehe hiyo, na kutangaza kuzinduliwa rasmi kwa mfumo wa saitelaiti wa kuongoza mawasiliano duniani wa Beidou No. 3.

  "Natangaza kuwa mfumo wa saitelaiti wa kuongoza mawasiliano duniani wa Beidou No. 3 umezinduliwa rasmi."

  Baada ya tangazo hilo, mfumo wa Beidou No. 3 ambao ni miundombinu muhimu ya anga za juu iliyojengwa na kuendeshwa na China kwa kujitegemea, umezinduliwa rasmi.

  Tangu mwishoni mwa mwaka 2018, mfumo wa Beidou No. 3 ulianza kutoa huduma kote duniani. Akiulizwa kuwa baada ya ujenzi wa mfumo huo kukamilika, huduma utakazotoa zitakuwa na tofauti gani na zamani? Naibu mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi Katika Anga za Juu iliyo chini ya Shirikisho la Kimataifa la Safari za Anga za Juu Bw. Yang Yuguang anasema:

  "Kama tunavyojua, kuanzia kizazi cha kwanza cha mfumo wa Beidou, ulikuwa na huduma ya Ujumbe Mfupi. Hivi sasa huduma hiyo imekuwa na uwezo mkubwa zaidi. Zamani tulikuwa tunaweza tu kutuma ujumbe wa kimaandishi wa maneno mia moja hivi tu, lakini hivi sasa tumeweza kutuma picha na hata sauti kupitia mfumo huo."

  Hivi sasa, mfumo wa Beidou unaweza kutoa huduma ya kutambua mahali ulipo kwa kiwango cha usahihi kisichozidi mita kumi. Bw. Yang Yuguang ameeleza kuwa, mfumo wa Beidou No. 3 utaweza kutoa huduma bora na nyingi zaidi. Kwa mfano una uwezo mkubwa zaidi wa kuongoza mawasiliano ya ardhini kwenye viwanja vya ndege, haswa kwenye hali mbaya ya hewa, ambao utahakikisha ndege zinaweza kutua kwa kujiendesha na kuongeza usalama wa ndege zinapotua. Bw. Yang Yuguang anaona, baada ya ujenzi wa mfumo wa Beidou No. 3 kukamilika, wateja kote duniani wataweza kunufaika na huduma zenye ubora na usahihi wa kiwango cha juu.

  "Naona katika siku zijazo, simu zetu za mikononi na zana nyingine za kielektroniki zote zitaweza kujumuisha mifumo mbalimbali ya kutambua mahali na kuongoza mawasiliano kama vile Beidou, GPS, Glonass na hata Galileo, ili kuinua kiwango cha usahihi wa huduma. Wateja wataweza kuchagua na kutumia ishara za mifumo mingine ya saitelaiti, na hivyo kuongeza kiwango cha utulivu, usalama na uhakika cha huduma hizi."

  Bw. Yang Yuguang pia amesema anatarajia kuwa katika siku zijazo mfumo wa Beidou No. 3 utatumiwa kwenye nyanja nyingi zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako