• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mvutano kuhusu uchaguzi wa shirikisho la Soka Kenya waendelea

    (GMT+08:00) 2020-07-31 17:44:57

    Aliyekuwa mkuu wa Shirikisho la soka la Kenya (FKF) Sam Nyamweya ametaka kuwepo na mazungumzo ili kutatua mvutano uliopo kwenye uchaguzi wa shirikisho la soka la Kenya. Msimamo wa Bw. Nyamweya unaungwa mkono na Herbert Mwachiro ambaye amekuwa akikosoa utaratibu ulipo sasa kwenye Soka ya Kenya ambaye pia alijaribu kugombea nafasi ya kuliongoza shirikisho hilo na kumwondoa mkuu wa sasa Nick Mwendwa. Sam Nyamweya, ambaye sasa anaonekana wazi kuitaka kazi yake ya zamani, pia amefafanua kuwa ni lazima kuwe na mchakato wa uchaguzi huru na wa haki utakaokubaliwa kwa wadau wote wa soka wa Kenya. Uchaguzi ndani ya KFK uliofanyika mara mbili katika miezi saba iliyopita ulibatilishwa na Baraza la kutatua Migogoro kwenye sekta ya Michezo (SDT), ambalo mwenyekiti wake John Ohaga alisema chaguzi zote mbili hazikukidhi mahitaji ya kuwa huru na haki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako