• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marefa watano tayari wamechaguliwa kuchezesha mechi ya Simba na Azam FC jumapili

  (GMT+08:00) 2020-07-31 17:45:49

  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi wametaja marefa watakaochezesha Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayochezwa Jumapili katika Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa. Tayari kikosi cha Namungo FC kipo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa tangu jana kwa ajili ya kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya Lindi kutwaa taji hilo, wakati Simba SC wao siku mbili hizi nao watasafiri kwenda Sumbawanga kwa ajili ya mechi hiyo. Azam Sports Federation Cup (ASFC) ni michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania ambayo bingwa wake hushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Lakini kwa mwaka huu Namungo imejihakikishia kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani hata kama itafungwa, kwani tayari Simba SC ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo na 21 jumla ambao watacheza Ligi ya Mabingwa katika msimu ujao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako