• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Morrison akamatwa na Polisi baada ya kujaribu kuleta jeuri

    (GMT+08:00) 2020-07-31 17:46:08

    Matukio ya utata na utovu wa nidhamu yanazidi kumwandama mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison baada ya kukamatwa na askari polisi kisha kuachiwa baadaye. Tukio hilo linadaiwa kutokea jana mchana baada ya askari wa doria waliolitilia shaka gari la mchezaji huyo kisha kutaka kulipekua sehemu iliyokuwa limeegeshwa na Morrison kugoma na kusababishwa kupelekewa polisi. Askari walihisi harufu ya kitu kutoka ndani ya hiyo gari sasa walipotaka kumfanyia upekuzi akagomea upekuzi huku akileta utata akitaka kuwarekodi polisi. Lakini baadaye polisi walifanikiwa kumsihi waelekee kituo cha polisi kwa hatua zaidi akakubali na akatoa maelezo yake kituo cha Polisi Oysterbay. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Edward Bukombe alithibitisha kushikiliwa kwa Morrison. Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Patrick Simon amesema kutokana na matukio ya Bernard Morrison ya utovu wa nidhamu amepelekwa kwenye Kamati ya Maadili. Morrison hajajiunga na timu kwa sasa ambapo mara ya mwisho kuonekana akiwa na Yanga ilikuwa ni Julai 12, Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba. Baada ya mchezo huo ambapo Morrison alitolewa dakika ya 64 na nafasi yake kuchukuliwa na Patrick Sibomana aliondoka jumla uwanjani na kwa sasa amekuwa akionekana akicheza mechi za mchangani huku akieleza kuwa anahofia kupigwa ikiwa anakwenda mazoezini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako