• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Corona yavuruga maandalizi ya Idd-ul-Adha

    (GMT+08:00) 2020-07-31 18:20:50

    Shughuli chache zilishuhudiwa Jumatano wakati Waislamu walianza kujiandaa kwa sherehe za Idd-ul-Adha ambazo zitafanyika Ijumaa.

    Waziri wa Usalama wa Nchi, Dkt Fred Matiang'i alitangaza rasmi kwamba Ijumaa itakuwa ni sikukuu ya kitaifa ili kutoa nafasi kwa Waislamu nchini kufanikisha sherehe hizo muhimu.

    Kutokana na athari za ugonjwa wa Covid-19 kimataifa, Waislamu waliohojiwa na radio China Kimataifa walisema hawatakuwa na uwezo wa kusherehekea jinsi ilivyokuwa kawaida katika miaka iliyopita.

    Kawaida siku tatu kabla ya sherehe hiyo, Waislamu hufurika katika masoko mbali mbali kujinunulia bidhaa kama nguo, vyakula na mnyama wa kuchinja. Hata hivyo, mwaka huu makumi tu ya waumini ndiyo wanaonekana sokoni walifanya matayarisho

    Sikukuu hiyo ambayo husherehekewa kila mwaka baada ya ibada ya Hijja mjini Mecca, huhusisha waumini hao kuchinja mfugo wa miguu minne kwa kumbukumbu ya Nabii Ibrahim aliyekuwa ameagizwa kumchinja mwanawe Ismael.Wafanya biashara wengi wa mifugo wanasema sikuu ya mwaka huu haina faida kubwa ikilinganishwa na za nyuma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako