• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Tanzania kudhibiti sumukuvu kwenye mazao

  (GMT+08:00) 2020-07-31 18:21:15

  Serikali ya Tanzania imetoa jumla ya dola za Marekani milioni 35.3 kwa ajili ya kupambana na tatizo la sumukuvu kwenye mazao ya wakulima nchini humo.

  Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya, amesema utafiti unaonyesha mazao ya karanga na mahindi ndio yanayoshambuliwa zaidi na sumukuvu hapa nchini.

  Kusaya alisema kuwa sumukuvu inatokana na kutofuatwa kwa hatua sahihi kwenye upatikanaji wa mbegu, upandaji, upaliliaji, uvunaji na wakati wa kuhifadhi mazao hayo baada ya mavuno.

  Alisema serikali ya Tanzania itajenga kituo cha umahiri wilayani Kongwa kitakachokuwa ni sehemu muhimu katika sekta ya kilimo kwa kutoa taaluma mbalimbali za kilimo.

  Pia alisema kupitia Mradi wa TANIPAC, halmashauri 12 zitajengewa maghala 12 na mawili visiwani Zanzibar ili kusaidia wakulima kuhifadhi mazao yao.

  Kusaya alisema kuwa serikali kupitia wataalamu wake wataendelea kutoa elimu kwa Watanzania ili kupata uelewa kwa jamii juu ya kuhifadhi mazao yao kwa ufasaha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako