• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Safaricom yamteua mwenyekiti mpya wa bodi

    (GMT+08:00) 2020-07-31 18:21:37

    Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imemteua afisa wao wa zamani Michael Joseph kama mwenyekiti mpya wa bodi yake.

    Bw Joseph alichukua wadhifa huo kutoka kwa Nicholas Ng'ang'a ambaye amekuwa uongozini tangu 2007, akiwa amehudumu kwa miaka 13.

    Vilevile Bw Ng'ang'a amekuwa kwenye bodi ya Safaricom, kwa muda wa miaka 16 baada ya kujiunga kama mwanachama mnamo 2004.

    Akitangaza uteuzi huo, Afisa Mkuu Mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa amesema Bw Joseph atachukua wadhifa huo rasmi Agosti 1, 2020, huku jukumu lake kubwa likiwa kujenga brandi ya kampuni na kuivumisha ili iendelee kupata faida.

    Taarifa ya kampuni hiyo imesema Joseph ana ujuzi na ufahamu mpana kufuatia mchango wake wa awali kwenye kampuni hiyo. Taarifa hiyo iliongeza kuwa Bw Joseph anaelewa sana Safaricom kuwa kuwa alihudumu kama afisa mkuu mtendaji mara mbili na pia mwanachama wa bodi yake kwa miaka kadhaa.

    Wakati wa uongozi wake ndipo Safaricom ilizindua mfumo wa kutuma na kupokea fedha maaarufu kama Mpesa ambayo imenufaisha wengi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako