• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Asilimia 70 ya dhahabu yatoroshwa kinyemela Tanzania

  (GMT+08:00) 2020-07-31 18:21:58

  Asilimia 70 ya dhahabu inayochimbwa kwenye machimbo ya Gasuma, Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, hutoroshwa kinyemela na baadhi ya wanunuzi, hali inayodaiwa kuukosesha mkoa huo mapato yatokanayo na madini hayo.

  Ofisa Madini mkoani humo Chacha Megewa amesema Idara ya Madini hupokea asilimia 30 pekee ya dhahabu inayouzwa mkoani humo huku madini mengi yakitoroshwa kwenda kuuzwa nje ya Simiyu.

  Utoroshaji huo alisema unafifisha mapato ya serikali mkoani humo na kuwaomba wachimbaji na wanunuzi kutii sheria kwa kuuza mali hiyo katika soko mkoani humo.

  Alisema Idara ya Madini imeamua kutenga eneo kwa ajili ya kujenga ofisi za wanunuzi wa dhahabu mgodini hapo, na tayari ujenzi wake umeshaanza rasmi.

  Baadhi ya wachimbaji na wanunuzi wa dhahabu katika mgodi huo wa Gasuma, walisema utoroshwaji huo unatokana na kudhorota kwa bei ya madini mkoani humo.

  Kwa mujibu wa wafanyabiashara mkoani humo, bei ya dhahabu katika Mkoa wa Simiyu ni ndogo, ikilinganishwa na masoko ya Mwanza, Mara na Geita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako