• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Raia wanane wauawa na wengine 30 wajeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu mashariki mwa Afghanistan

  (GMT+08:00) 2020-07-31 18:23:44

  Raia wanane wameuawa na wengine 30 wamejeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu lililotegewa kwenye gari, uliotokea jana katika jimbo la Logar Mashariki mwa Afghanistan.

  Mlipuko huo ulitokea jana jioni, na habari za awali zilisema watu 8 waliuawa na wengine 30 walijeruhiwa, na miongoni mwa wahanga kuna watoto. Lakini duru za habari jimboni humo zimesema watu 15 waliuawa na wengine 35 walijeruhiwa, na kuwa wanajeshi ni miongoni mwa watu walioathiriwa na mlipuko huo. Mlipuko huo umetokea kabla ya kusimamishwa vita kati ya wapiganaji wa kundi la Taliban na vikosi vya usalama, ambao wamekubaliana kusitisha vita kwa muda wa siku tatu, kwa ajili ya sikukuu ya Idi el Adha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako