• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Msumbiji azindua mpango wa kuhimiza kilimo

  (GMT+08:00) 2020-07-31 18:24:03

  Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji amezindua mpango wa "Sustenta" wenye lengo la kuwaunganisha wakulima wadogo wadogo kwenye minyororo ya uzalishaji wa kilimo na kuhimiza kilimo endelevu, ili kuongeza tija na kipato kwa wakulima.

  Mpango wa Sustenta ulianzishwa mwaka 2017 kwenye wilaya 10 katika majimbo ya Nampula na Zambezia, na sasa uko kwenye awamu ya pili inayohusisha nchi nzima.

  Rais Nyusi amesema huu ni mpango wa kihistoria na serikali itatenga asilimia 10 ya bajeti yake kwa ajili ya sekta ya kilimo, ili kuhakikisha Msumbiji inajitosheleza kwa chakula na kuondokana na njaa. Mpango huo unahimiza uzalishaji wa vyakula vinavyotumiwa zaidi hasa mahindi, maharage, na uzalishaji wa kuku, mayai, sukari, muhogo, mboga za majani na matunda.

  Kilimo kikiwa ni uti wa mgongo wa uchumi wa Msumbji, kinachangia asilimia 25 ya pato la taifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako