• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mfumo wa Beidou No. 3 kufungua ukurasa mpya wa huduma za uongozaji wa safari duniani

  (GMT+08:00) 2020-07-31 20:12:52

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, uzinduzi rasmi wa mfumo wa Beidou No.3 utafungua ukurasa mpya wa huduma za uongozaji wa safari duniani.

  Bw. Wang amesema mfumo wa Beidou si kama tu ni mfumo wa China, bali pia ni mfumo wa dunia nzima, na si kama tu utahudumia China, bali pia itahudumia dunia nzima. Ameongeza kuwa mfumo huo utatoa huduma za uongozaji wa safari, mawasiliano ya ujumbe, na uokoaji wa kimataifa, hivi sasa mfumo wa Beidou unaweza kufika kwenye zaidi ya nchi na sehemu 200, na nusu ya nchi duniani zimeanza kutumia mfumo huo.

  Amesisitiza kuwa China inapenda kuendelea kuongeza mawasiliano na ushirikiano na jumuiya ya kimataifa katika sekta ya safari za anga za juu, kwa kufuata kanuni ya kuheshimiana, kufunguliana mlango, kunufaishana, na usawa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako