Rais Xi Jinping wa China leo ametoa salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Tanzania Rais John Pombe Magufuli kutokana na kifo cha rais wa zamani wa nchi hiyo Benjamin William Mpaka.
Katika salamu zake, Rais Xi amesema, Benjamin Mkapa alikuwa ni kiongozi hodari wa Tanzania na Afrika, na pia alikuwa ni rafiki mkubwa wa watu wa China ambaye alitoa mchango muhimu katika maendeleo ya uhusiano kati ya China na Tanzania, na kati ya China na Afrika.
Rais Xi amesema anatilia maanani maendeleo ya uhusiano kati ya China na Tanzania, na anapenda kushirikiana na Rais Magufuli kusukuma mbele uhusiano kati ya China na Tanzania, ili kunufaisha nchi hizo mbili na watu wao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |