• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Kenya kufanyia marekebishao uamuzi wa kuzuzia Watanzania kuingia nchgini humo

  (GMT+08:00) 2020-08-03 16:51:32
  Serikali ya Kenya Jumamosi ilijikakamua kurekebisha uhusiano wake na Tanzania baada ya ndege za Kenya Airways kupigwa marufuku kuingia katika nchi hiyo.

  Uamuzi wa Tanzania kupiga marufuku ndege za Kenya ulitokana na kuwa serikali haikuijumuisha katika orodha ya mataifa ambayo yaliruhusiwa kuja nchini bila masharti makali.

  Waziri wa Uchukuzi, James Macharia, alisema alijadiliana na mwenzake wa Tanzania na akamfafanulia kuhusu kanuni hizo za Kenya.

  Kulingana naye, hakuna nchi iliyopigwa marufuku kuja Kenya, bali kanuni ni kwamba watu kutoka mataifa kadhaa ambayo hayakuwa kwenye orodha iliyotolewa watahitajika kukaa karantini wakija nchini.

  Kenya Airways ilikuwa imepanga safari moja kuelekea Dar es Salaam siku ya Ijumaaa ikirejelea usafiri wa kimataifa, lakini ikalazimika kuifutilia baada ya amri hiyo ya Tanzania.

  Awali, Waziri Msaidizi katika Wizara ya Mashauri ya Kigeni, Bw Ababu Namwamba alikana kuwa kuna tofauti za kidiplomasia kati ya Kenya na Tanzania.

  Bw Namwamba alisema uhusiano baina ya Nairobi na Dar es Salaam ni shwari, japo akidokeza kuwa ikiwa kuna tatizo lolote kuna mbinu za kulitatua. Kumekuwepo na hofu kwamba vita hivi baridi kati ya mataifa haya mawili, huenda vikaathiri pakubwa sana sekta ya biashara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako