• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la filamu la kimataifa la Shanghai lafungwa

    (GMT+08:00) 2020-08-03 17:02:41

    Tamasha la 23 la filamu la kimataifa la Shanghai lililofanyika kwa siku 9 lilifungwa rasmi jana tarehe 2.

    Ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, kwa mara ya kwanza tamasha hilo lilifanya maonesho ya filamu kwenye majumba ya sinema, sehemu za nje na mtandao wa internet, na kuwakutanisha watazamaji zaidi laki 1.6 na idadi ya watu walioingia sinema kutazama filamu ilizidi laki 1.47.

    Kutokana na mwongozo uliotolewa katika kipindi hiki cha kukinga na kudhibiti maambukizi ya Corona, tiketi za tamasha hilo ziliuzwa kwenye mtandao wa internet, na majumba 29 ya sinema mjini Shanghai yalionesha filamu zaidi 320 za China na nchi za nje.

    Maonesho ya filamu kwenye sehemu za nje yalifanyika kwenye maeneo 7 ya kibiashara na mitaa zaidi 30 mjini Shanghai, na filamu mpya za nchi kadhaa za Ukanda Mmoja na Njia Moja pia zilioneshwa kwenye sehemu za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako