• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbunge apendekeza pesa zaidi kwa kilimo

    (GMT+08:00) 2020-08-04 20:10:18
    MWENYEKITI wa kamati ya Kilimo katika Bunge la Kitaifa, Bw Sila Tiren, ameirai serikali kuu iongeze kiasi cha fedha kwenye bajeti kinachotengewa sekta hiyo hadi asilimia 10.

    Amesema itasaidia kuongezea nchi mapato kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha kuwa wakulima wananufaika na kuongezea taifa uzalishaji wa vyakula vya kutosha.

    Pia mgao mkubwa wa kifedha kwa kilimo, utahakikisha utekelezaji wa ajenda kuu nne za serikali zinatimia.

    Mbunge huyo pia alieleza kushangazwa kwake na uamuzi wa serikali wa kuongeza ushuru unaotozwa kwenye pembejeo za kilimo hadi asilimia 14, akisema atashauriana na Waziri Peter Munya kuhusu suala hilo.

    Katika bajeti ya 2020/2021, serikali ilitengea sekta ya kilimo Sh52.1 bilioni huku ushuru ukiondolewa kwenye mauzo ya mahindi kati ya mageuzi mengine ya kuhakikisha kuna chakula cha kutosha nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako