• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki ya Uganda imeweka vigezo vinne ili kuifanya Uganda kuwa nchini ya kieletroniki.

  (GMT+08:00) 2020-08-04 20:11:13
  Benki ya Uganda imeweka vigezo vinne ambavyo vina tayarajiwa kuifanya Uganda kuwa nchini ya kieletroniki.

  Bi Charity Mugumya, mkurugenzi wa mawasiliano katika Benki ya Uganda, amesema Benki Kuu imeweka madhumuni manne ya mikakati, miongoni mwao kukuza malipo ya elektroniki na benki ya matandaoni kama njia moja kuu ya uchumi wa kieletroniki .

  Malengo mengine, amesema, ni pamoja na kutekeleza mkakati wa kitaifa wa kuingiza kifedha ambao unajumuisha kujenga miundombinu ya kidijitali, kutekeleza mkakati wa elimu ya na kufanya huduma za malipo kuwa nafuu.

  Mnamo Agosti mwaka jana, Benki Kuu ya Uganda ilielekeza watoa huduma ya malipo ya kadi za elektroniki kuondoa malipo ya ziada shughuli ilizofanywa kwa njia ya elektroniki wakati wa mauzo.

  Benki Kuu imesema, itasaidia kufanya malipo ya elektroniki kuwa ya bei nafuu zaidi na ya kuhitajika.

  Benki Kuu, chini ya sera ya Mifumo ya Ulipaji ya Taifa, ilikuwa imeweka 2022 kama mwaka ambao Uganda inapaswa kufanikiwa kiuchumi na kufanya shughuli zake zote za kifedha kwa njia ya kieletroniki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako