• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wamiliki wa baa wa Rwanda wabadilisha mtindo wa biashara kutokana na COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-08-05 09:24:07

  Wamiliki wa baa nchini Rwanda wamebadilisha mtindo wa biashara ili kuendana na mazingira ya mapambano dhidi ya virusi vya Corona. Baada ya serikali ya Rwanda kutoa agizo la biashara kufanya kazi zikiwa na wahudumu wa kimsingi, baadhi ya wamiliki wa baa wamebadilisha baa zao na kuwa migahawa.

  Kutokana na kuwa baa hizo zilikuwa na samani na vyombo vya kulia chakula, haikuwa vigumu kwa baa kubadilishwa kuwa migahawa. Hata hivyo, licha ya kuwa kubadilisha baa kuwa mgahawa haikuwa kazi ngumu, hii haina maana kuwa wateja wa baa walibadilika na kuwa wateja wa chakula. Mmiliki mmoja amesema mapato yake kwenye mgahawa yamepungua kwa asilimia 60 ikilinganishwa na wakati biashara yake ilipokuwa baa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako